2 Februari 2026 - 22:08
Afisa Mstaafu wa Jeshi la Marekani: Iran Isiamini Tena Marekani +Video

Afisa mstaafu wa jeshi la Marekani amesema Iran haipaswi tena kuiamini Marekani. Lawrence Wilkerson: “Kama ningekuwa Iran, nisingekubali tena kufanya mazungumzo na Washington.” Ameonya kuwa sera za Marekani zimejaa usaliti na kuziamini huleta gharama kubwa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kanali Lawrence Wilkerson, afisa mstaafu wa jeshi la Marekani, ameikosoa vikali sera za Washington na kusema:
Kama ningekuwa nafasi ya Iran, kwa hali yoyote nisingeingia tena katika mazungumzo na Marekani.”

Ameongeza kuwa:

 “Sera za Marekani katika uwanja wa kimataifa zimejaa kutokuaminika na usaliti, na uzoefu wa zamani unaonyesha wazi kuwa kuiamini Washington kunaleta gharama kubwa.”

Your Comment

You are replying to: .
captcha